Araghchi aliyasema hayo katika hotuba yake kwenye mkutano wa 17 wa kilele wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi BRICS mjini Rio de Janeiro, Brazil, jana Jumapili. Amesema "mashambulio ya kijeshi na ya kigaidi" ya utawala wa Israel ya siku 12 yalifanywa kwa uungaji mkono, ushirikiano na hatimaye ushiriki wa Marekani.
Ameongeza kuwa, shambulio hilo haramu la Israel dhidi ya Iran limekiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambapo watu zaidi ya 6,000 wasio na hatia waliuawa na kujeruhiwa, mbali na kuharibu miundombinu, maeneo ya makazi na vituo vya nyuklia nchini Iran.
"Mashambulizi ya Marekani-Israel dhidi ya vituo vyetu vya nyuklia yalikiuka wazi NPT na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo liliidhinisha makubaliano ua nyuklia ya Iran mwaka 2015," mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran amesisitiza.
"Kujihusisha Marekani katika uvamizi huu kwa kulenga vituo vya kiraia vya nyuklia vya Iran kumefuta shaka juu ya ushiriki kamili wa serikali ya Washington katika vita vya kivamizi vya Israel dhidi ya Iran," ameongeza Araghchi.
Mnamo Juni 13, Israel ilianzisha uchokozi wa wazi na usio na msingi dhidi ya Iran, na kuwaua makamanda kadhaa wa ngazi za juu wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia wa nchi hii.
Tarehe 22 Juni, Marekani ilijiunga rasmi na vita hivyo vya kichokozi vya Israel dhidi ya Iran, kwa kutekeleza mashambulizi kwenye vituo vitatu vya nyuklia hapa nchini, kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa na mkataba wa NPT.
Your Comment